NJIA ZA KUMWANDAA MTOTO KUWA NA UPEO MKUBWA(AKILI)
Watoto ni wepesi kushika vitu na ni waelewe sana
,wanakuwa kulingana na malezi wanayopewa na wazazi. Wazazi wengi wanaamini
mtoto huanza kufunzwa akiwa miaka 3-4 hapana tunakosea sana wenzetu
nchi zilizo endelea wanaanza funza watoto wakiwa na miezi 6 hufunzwa kila vitu
kulingana na umri mfano kusomewa vitabu mzazi unaweza ukaona haelewi hapana
kichwa kinazoea kile anachofunzwa mara kwa mara .
Ukimwandalia mtoto msingi mzuri tangu udogoni basi ana nafasi nzuri ya kuwa
na upeo(akili) na uwelewa mkubwa.Wazazi
wengi wanaachia watoto wakiamini kila kitu watafunzwa shule ,hapana ni makosa
mzazi inakubidi uchukue nafasi yako
pia kuhakikisha unampa mwongozo
bora mtoto .
Watoto wengine ni wazito kuelewa ️au
kushika vitu kwa haraka hivyo vizuri akanza kufunzwa mapema.Maandalizi mazuri
kwa mtoto yatamjenga kiakili na kumfanya kuwa bright. Hakuna mtoto mjinga
duniani ni wazazi tu kukosea kuto kuwapa misingi bora watoto tangu wakiwa na
umri mdogo.
ujue ratiba yake akitoka shule anatakiwa kufanya
nini,atacheza na wenzake kupumzisha kichwa kumbuka michezo ni muhimu
kiafya,baada ya michezo afanye kazi za shule kwa kumsaidia,muulize leo shule
wamefanya nini ?kipi kilimfurahisha? nini kilimkasirisha? ,masomo yalikuwaje
itakusaidia kujua maendeleo yake ya shule na mahusiano yake na walimu na
wanafunzi wenzake ,na unaweza mwelekeza homework yake
Wale wadogo wasio enda shule miezi 9-mpaka miaka 3 nao vile vile anatakiwa tengewa mda Wake ,anavyozidi kukua anazoea ile ratiba na kukaa kichwani kwamba nitacheza ila kunamda nitakaa kusoma hata kama dakika 10-20
0 comments:
Post a Comment