Random Post

Tuesday, March 15, 2016

TUPANDE MITI YA MATUNDA

TUPANDE MITI YA MATUNDA KUKIDHI KIWANGO KINACHOHITAJIKA KWA SIKU.

Kila hatua utakayochukua ya kula zaidi matunda na mboga mboga, itakusaidia wewe na familia yako kuwa na afya njema. Hii ni kwa sababu matunda na mboga za majani yana viini lishe muhimu ambavyo husaidia ufanyaji kazi wa mifumo ya miili yetu na kutukinga na aina mbali mbali za magonjwa.

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO, ni kuwa ulaji wa angalau gramu 400(pungufu kidogo ya nusu kilo) za matunda na mboga kwa siku zinatuepusha na hatari ya kupata magonjwa yanayosumbua jamii nyingi duniani hivi leo. Magonjwa haya zaidi ni yale yasiyo ya
uambukizi kama kisukari, shinikizo la damu, kiharusi na mengine mengi. Pia ulaji wa matunda na mboga mboga utatusaidia kupata  viini lishe kama fiba, vitamini, madini katika viwango sahihi vinavyohitajika kwa siku.

Katika nchi zinazoendelea ambapo walio wengi wanaishi chini ya dola moja kwa siku, ni vigumu kuweza kumudu kufikia kiwango kilichopendekezwa na shirika la afya duniani, lakini hii isitufanye kushindwa kumudu kiwango kilichopendekezwa. Tunaweza kujitosheleza kwa matunda na mboga za majani kwa kuotesha miti ya matunda mbali mbali majumbani mwetu, pia kuwa na bustani za mboga mboga. Hii itatusaidia kuweza kufikia kiwango kinachopendekezwa na shirika la afya WHO na kuboresha afya zetu.

Ili kuboresha kiwango kinachohitajika cha matunda na mboga mboga, basi hatuna budi kufanya

yafuatayo:-
  • Tuhakikishe kuwa nyumbani kwetu hapakosekani bustani za mboga na matunda.
  • Kila wakati hakikisha katika mlo wako haukosi mboga za majani.
  • Hakikisha haukosi matunda ya kila msimu, mfano embe, nanasi, chungwa, mastafeli, papai, fenesi,parachichi na mengineyo mengineyo mengi.
  • Kula aina tofauti za matunda na mboga za majani

0 comments:

Post a Comment