FAIDA NYINGI ZA PAPAI.
Mpapai ambao kitaalam hujulikana kama Carica papaya, ni mti wenye tunda lenye virutubisho vingi ambao una asili na hulimwa na kustawi katika nchi za kitropiki. Mpapai hukua hadi kufikia kimo cha mita 10. Mti huu huwa na makovu ambayo hutokana na majani ya mpapai yaliyoanguka unapokua.
Mpapai ni wenye asili ya bara la Amerika ya kati na kusini lakini badae mmea wa tunda hili ulisambaa katika visiwa vya Caribbean, Florida na Baadhi ya nchi za Afrika. Leo hii papai hulimwa katika nchi za India, Australia, Indonesia, Philippines, Malaysia, U.S na Hawaii.
Mmea huu wenye jinsia tatu: jike, dume na jikedume(hermaphrodite). Mpapai dume huzalisha poleni (mbegu dume) lakini hauzai matunda. Mpapai jike hauwezi kuzaa matunda bila kurutubishwa na poleni kutoka mpapai dume. Mpapai dumejike hujitegemea na waweza kuzaa matunda wenyewe. Na mipapai yote inayolimwa kibiashara huwa ni dumejike. Tunda la papai lina kirutubisho cha beta carotene ambacho hulipa papai rangi nzuri ya chungwa ya kung'aa.
Virutubisho katika papai
Jedwali likionyesha kiasi cha virutubisho katika gramu 100 za papai.
Aina ya kirutubisho
|
Kirutubisho
|
Kiwango kilichopo
|
Vitamini
|
Vitamini A
|
135ug
|
Vitamini E
|
1 ug
| |
Vitamini C
|
62 mg
| |
Thiamine
|
0.0mg
| |
Niacini
|
0.3mg
| |
Vitamini B 6
|
0.0mg
| |
Folate
|
38 ug
| |
Madini
|
Kalshamu
|
24mg
|
Phosphorasi
|
5 mg
| |
Magnesiamu
|
10mg
| |
Potasiamu
|
257mg
| |
Munyu (Sodium)
|
3mg
| |
Chuma
|
0.1mg
| |
Zinki
|
0.1mg
| |
Shaba
|
0.0mg
| |
Manganizi
|
0.0mg
| |
Protini muhimu
|
TRP(Tryptophan)
|
8mg
|
THR(Threonine)
|
11mg
| |
ILE(Isoleucine)
|
8 mg
| |
LEU(Leucine)
|
16mg
| |
LYS(Lysine)
|
25mg
| |
MET(Methionine)
|
2 mg
| |
CYS(Cysteine)
|
5 mg
| |
PHE(Phenylalanine)
|
9 mg
| |
TYR(Tyrosine)
|
5mg
| |
VAL(Valine)
|
10 mg
|
Papai hupunguza kiwango cha lehemu kwa kuwa lina Vitamini C na virutubisho vingine ambavyo huzuia kujijenga kwa lehemu katika mishipa ya damu ya ateri. Lehemu inapojikusanya kwa wingi katika ateri, mishipa hii ya damu huwa na njia nyembamba au kuziba na kusababisha kuongezeka shinikizo la damu na hata shambulizi la moyo.
Tunda hili husaidia kupunguza uzito wa mwili, papai lina fiba (nyuzi lishe) ambazo husaidia kupunguza uzito, unapokula tunda hili, fiba husababisha kujisikia umeshiba kwa hiyo mtu hupunguza kiasi cha chakula chenye nishati nyingi ambapo hupelekea kupunguza uzito wa mwili.
Katika utafiti mmoja uliochapishwa katika jarida la magonjwa ya viungo(arthritis) ulionyesha kuwa, watu wanaokula vyakula vyenye kiwango kidogo cha vitamini C walikuwa katika hatari mara tatu zaidi ya kupata magonjwa ya viungo. Kula papai ni muhimu kwa afya ya mifupa yako kwa kuwa husaidia kuondoa visababishi vya uvimbe na maumivu pia lina vitamini C kwa wingi ambayo hutukinga na aina nyingi za magonjwa ya viungo.https://www.blogger.com/blogger.g?blogID=4190877296945965391#editor/target=post;postID=8284290276971163185
0 comments:
Post a Comment