Tikiti maji ni tunda ambalo kisayansi hujulikana kama
Citrullus lanatus katika familia ya
Cucurbitaceae, ambalo mmea wake hutoa maua na humea kwa kutambaa. Mmea huu ambao hutoa matunda makubwa yaliyo na umbo la tufe au yai, asili yake ni huko kusini mwa Afrika.
Ushahidi wa kihistoria ulionyesha kuwa mmea huu ulilimwa huko Misri tangu milenia ya pili BC, na katika karne ya kumi AD mmea wa tikiti maji ulikuwa umesambaa huko bara Hindi hata Mashariki ya mbali.Lakini hapo badae ulimaji
wake ulifika huko Ulaya ya kusini na kusambaa duniani kote.Tafiti nyingi zimekuwa zikifanyika kujaribu kuzalisha mbegu za tikiki zenye kukabiliana na magonjwa yashambuliayo mmea huu.
Ijapokuwa watu wengi huamini kuwa tikiti maji ni tunda lililo na maji na sukari peke yake, lakini ukweli ni kuwa tunda hili lina aina nyingi ya virutubisho , mfano vitamini, madini na viondoa sumu(antioxidants).
Jedwali likionyesha kiasi cha virutubisho katika gramu 100 za tikiti maji.
Aina ya kirutubisho
|
Kirutubisho
|
Kiwango kilichopo
|
Vitamini
|
Vitamini A
|
28µg
|
|
Vitamini E
|
0.0 µg
|
|
Vitamini C
|
8.1mg
|
|
Thiamine
|
0.03mg
|
|
Niacini
|
0.2mg
|
|
Vitamini B 6
|
0.045mg
|
|
Folic acid
|
3mg
|
Madini
|
Kalshamu
|
7mg
|
|
Phosphorasi
|
11mg
|
|
Magnesiamu
|
10mg
|
|
Potasiamu
|
112mg
|
|
Munyu (Sodium)
|
1mg
|
|
Chuma
|
0.2
|
|
Zinki
|
0.1mg
|
|
Shaba
|
0.0mg
|
|
Manganizi
|
0.0mg
|
Protini muhimu
|
TRP(Tryptophan)
|
7.0mg
|
|
THR(Threonine)
|
27mg
|
|
ILE(Isoleucine)
|
19mg
|
|
LEU(Leucine)
|
18mg
|
|
LYS(Lysine)
|
62mg
|
|
MET(Methionine)
|
6mg
|
|
CYS(Cysteine)
|
2mg
|
|
PHE(Phenylalanine)
|
15mg
|
|
TYR(Tyrosine)
|
12mg
|
|
VAL(Valine)
|
16mg
|
|
ARG(Arginine)
|
59mg
|
|
HIS(Histidine)
|
6mg
|
Mbali na virutubisho vilivyoonyeshwa katika jedwali, tunda hili la tikiti maji pia lina viondoa sumu kama flavonoids, carotenoids na triterpenoids pia kiasi kikubwa cha maji,na virutubisho hivi hulifanya tunda hili kuwa na sifa ya vyakula vyenye faida kubwa mwilini.
Tafiti nyingi zimeonyesha kuwa, kuongeza matumizi ya vyakula vitokanavyo na mimea kama tikiti maji,matunda mengine na mbogamboga hupunguza hatari ya kupata magonjwa, kuboresha maisha na kuongeza umri wa kuishi. Twaweza kuepukana na magonjwa kama uzito mkubwa(obesity),kisukari na magonjwa ya moyo. Ulaji wa vyakula hivi humfanya mtu kuwa na afya njema,ngozi yenye afya,nywele na uzito ulio wa wastani.
Tunda hili lenye lycopene ambayo ni kiondoa sumu(antioxidant) na ambayo hulipa tunda hili rangi ya kupendeza iliyo nyekundu au pink, pia hupatikana katika nyanya na matunda mengine yaliyo na rangi nyekundu.
Tafiti za awali zimeonyesha kuwa watu walao matunda kama tikiti na mengineyo yenyelycopene kwa wingi waweza kuwa na nafasi ndogo ya kupata maradhi ya saratani hususani saratani ya tezi dume. Lakini hapajakuwepo kwa ushahidi ulio thabiti kuonyesha uhusiano uliopo kati ya saratani ya tezi dume na utumiaji wa matunda yenye lycopene ili kuweza kutambuliwa na mamlaka za chakula na tiba.
Katika utafiti mmoja uliochapishwa mwaka 2013 katika jarida la Kimarekani la shinikizo la damu, ulionyesha ulaji wa tikiti maji kwa watu wazima walio na uzito mkubwa uliweza kupunguza shinikizo la damu la aota (aortic BP).
L-citrulline ni aina ya protini iliyo katika tikiti maji na ambayo hubadilishwa mwilini katika figo na kuwa protini ijulikanayo kama
L-arginine.
L-citrulline pia huongeza utengenezwaji wa
nitric oxide, ambayo hufanya mishipa ya damu kutokukakamaa na kuboresha mzunguko wa damu mwilini na hii ndiyo sababu ya kupungua kwa shinikizo la damu. Tunda hili limejipatia umaarufu kwa wale walio katika ndoa,kwa kuwa
nitric oxide huongeza pia mzunguko wa damu katika viungo vya uzazi, kwa hiyo wale walio na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume kwa kiwango kidogo na kati, waweza kufaidika na tunda hili.
Kwa wana michezo ulaji wa tunda hili au juisi yake ni wa faida kubwa kwa kuwa husaidia kupunguza maumivu ya misuli na kuondokana na uchovu kwa haraka baada ya mazoezi au michezo ya kutumia nguvu. Watafiti wanaamini kuwa hii ni kwa sababu ya uwepo wa protini ya L-citrulline katika tikiti maji.
Tikiti maji ni tunda muhimu katika kurekebisha mmeng’enyo. Kwa kuwa tunda hili limetengenezwa na kiasi kikubwa cha maji na fiba husaidia kuondoa matatizo ya kukosa choo (constipation) na kuboresha mmeng’enyo wa chakula tumboni. Pia kwa kuwa tunda hili lina asilimia 92 ya maji na madini, huwa ni chaguo zuri kwa wagonjwa wenye upungufu wa maji mwilini.
Hatari ya kupata ugonjwa wa pumu ni mdogo kwa wale wanaokula aina fulani ya virutubisho. Katika moja ya virutubisho hivi ni vitamini C ambayo hupatikana katika aina nyingi za matunda na mbogamboga likiwemo tikiti maji.
Tikiti maji husaidia afya ya ngozi kwa kuwa lina vitamini A na C. Vitamini A husaidia katika ukuaji wa tishu za mwili,zikiwemo ngozi na nywele. Vitamini C husaidia katika utengenezaji wa kolageni mwilini na husaidia kupona haraka kwa tishu zilizo na majeraha ikiwemo ngozi.
Tahadhari
Tikiti maji siyo lishe iliyokamilika peke yake, pia siyo tiba itakayokufanya kuacha kufuata ushauri wa daktari. Ni vema basi kuhakikisha tunakula mlo ulio kamilika ili kujenga afya bora. Tunapopata matatizo mbali mbali ya kiafya ni vizuri pia kuonana na wataalamu wa afya kwa ajili ya utafiti, ushauri na kupata tiba iliyo sahihi.