Random Post

Ngoma za watoto

Baadhi ya watoto wa Shule za Msingi kutoka Wilaya ya Ilala wakionesha vipaji vya kucheza ngoma wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya sanaa yaliyoandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata),na kufadhiliwa na Kampuni ya Msama Promotions . Jumla ya watoto 200 wamenufaika na mafunzo hayo.

Ubunifu kwa watoto

Ubunifu kwa watoto ni jambo muhimu sana katika kuweza kuongeza ufahamu juu ya mambo mbalimbali na kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazomzunguka.

Teknolojia kwa watoto

Swala la teknolojia hususani ya computer ni muhimu kwa watoto ilikuweza kukabiliana na changamoto za ukuaji wa teknolojia.

Mazingira hatarishi kwa watoto

Watoto wanatakiwa kuwa mbali na mazingira hatarishi ambayo yanaweza kupelekea hatari za maisha yao na afya kiujumla.

Mtoto aliyetengeneza jezi ya Messi kwa mfuko wa plastiki atumiwa jezi na mpira.

Mtoto wa kiume mwenye uraia wa taifa la Afghanistan ambaye hivi karibuni aligonga vichwa vya mitandao ya kijamii kwa ku vaa fulana ya mfuko wa plastiki ilio na jina la Lionel Messi hatimaye amepata jezi nzuri kutoka kwa mshambuliaji huyo wa Argentina

Thursday, March 17, 2016

Food Poisoning (Kudhuriwa na chakula)


Food Poisoning (Kudhuriwa na chakula)


Wapenzi  wasomaji karibuni katika kipindi kingine cha Ijue Afya Yako. Kipindi ambacho lengo lake ni kujadili masuala mbalimbali yanayohusu afya na tiba ili kupata ufahamu zaidi juu ya kuimarisha afya zetu na ya jamii nzima kwa ujumla. Hii ni sehemu nyingine ya makala ya Ijue Afya Yako, ambapo tutazungumzia sumu inayopatikana ndani ya vyakula au kwa kimombo food poisoning, karibuni.
&&&&&&&&&&
Neno food poisoning au kudhuriwa na chakula ni tatizo linalotokea baada ya kula chakula au kunywa kinywaji kilichochanganyika na vijidudu au kitu chenye sumu au kuguswa na aidha sumu za bakteria na vimelea vinginevyo vya maradhi. Kwa ujumla hali hii hutokea baada ya mtu kula chakula kulichochafuliwa na matokeo ya hali hiyo ni mtu kupatwa na maumivu ya tumbo, tumbo kukata, kuharisha, kutapika na dalili nyinginezo. Kesi nyingi za kuchafuliwa huko kwa chakula zinatokana na ulaji wa vyakula vilivyochafuliwa na bakteria wenye kusababisha madhara. Hata hivyo food poisoning inaweza pia kusababishwa na virusi, kemikali, mimea na samaki wenye sumu. Kwa kawaida mazingira anayoishi binadamu yamezungukwa na vijidudu katika kila kona, kwa hiyo kutokea uchafuzi wa chakula ni jambo la kawaida huku baadhi ya vimelea hao pia wakiwa na manufaa kwa mazingira na pia binadamu. Tatizo la sumu inayotokana na chakula baadhi ya wakati hutishia maisha ya watu, na nchini Marekani pekee maisha ya mamilioni ya watu huwa hatarini kila mwaka kutokana na food poisoning.
Tatizo la food poisoning linaweza kusababishwa na vitu vifuatavyo:-
1. Bacteria: Campylobacter ndio bakteria wanaosababisha sumu kwenye vyakula kwa kiasi kikubwa na kumpelekea muathirika kuharisha. Bakteria huyo kwa kawaida hupatikana katika vyakula, maji au maziwa yasiyochemshwa na pia kupitia wanyama walioathirika. Bakteria wengine wanaosababisha tatizo hili ni Salmonella, E. coli, Shigella na aina ya Clostridia.
2. Parasite (vimelea): Amoeba na giardia pia huleta matatizo kwenye chakula. Vimelea hawa wanapatikana kwa kiasi kikubwa katika nchi zinazoendelea.
3. Virusi: Baadhi ya virusi kama rotavirus pia huleta matatizo kwenye chakula
4. Sumu au kemikali: Baadhi ya bakteria wanaweza kuchafua chakula hivyo kinapoliwa huleta madhara. Samaki kama tuna wana kiasi kikubwa cha madini ya zebaki au mercury hivyo wakiliwa na mama mjamzito huleta madhara kwa mtoto aliye tumboni. Vimelea hao wanaotuzunguka wanapatikana pia kwenye chakula na wakati mwingine wanaweza kuwa wa manufaa kwetu. Hata hivyo bakteria ambao wako katika vitu vilivyooza na mabaki ya vyakula, pia huleta madhara.
Lakini je chakula kinaweza kuchafuliwaje?
Chakula kinaweza kuchafuliwa wakati wa uzalishaji, kuhifadhiwa au kupikwa. Kwa mfano kutohifadhi chakula kwa usahihi au kwenye joto lililosahihi kama kutoweka chakula kwenye jokofu. Tatizo hili hutokea sana kwa vyakula vya jamii ya nyama, maziwa na samaki. Pia kutopika chakula sawasawa. Mara nyingi bakteria huwepo katika nyama mbichi hivyo isipopikwa na kuiva vizuri huweza kuleta madhara. Chakula pia kinaweza kuchafuliwa pale mwandaaji wa chakula asipofuata kanuni za afya na usafi. Maji pia yanaweza kuwa machafu pale bakteria au kinyesi cha binadamu na wanyama kinapoingia au kuchanganyika na maji. Tatizo hili hushuhudiwa sana katika nchi na mazingira yenye usafi duni. Katika nchi kama hizo, chakula pia kinaweza kutengenezwa ama kutayarishwa kwa kutumia maji yenye vimelea. Vyakula vinavyotokana na wanyama, vyakula vibichi na vile vya jamii ya mboga ambavyo havioshwi vyema, vyote vinaweza kuwa na vidudu maradhi na kuchafua chakula au kusababisha food poisoning. Backeria kama vile Salmonela na Listeria ni miongoni mwa vimelea vinavyopatikana katika vyakula vilivyoharibika au kuoza.
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&
Mtu aliyekula chakula kilichochafuliwa au kugusana na vijidudu maradhi hao huwa na dalili kuu zifuatazo: Kutapika, kuharisha, kichefuchefu na maumivu ya tumbo hali ambayo kitaalamu hujulikana kama stomach flu. Dalili kubwa ni kuharisha na wakati mwingine kutapika na tumbo kusokota. Maumivu hupungua kwa muda hasa baada ya kupata choo. Aidha dalili hizo mara nyingi huambatana na maumivu ya misuli, homa, kutetemeka mwili na kuhisi kuchoka. Hatua ya kuhara na kutapika muathirika husaidia mwili kuondoa mada zenye sumu au athari katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula (digestive tract) na hivyo kuzizuia sumu au vijidudu maradhi hivyo kuingia katika mfumo wa damu. Wakati mwingine inakuwa vigumu kueleza iwapo umepatwa na tatizo la food poisoning baada ya kula chakula kilichoharibika. Hivyo iwapo mtu atakuwa na mojawapo ya dalili hizo zilizotajwa, kama vile tumbo kukata na kuharisha ni vyema awaulize watu wengine wa familia iwapo kuna wengine walio na dalili kama hiyo na kama wamekula chakula kama hicho alichokula yeye. Wakati mwingine mtu huanza kujisikia mgonjwa katika muda wa masaa machache baada ya kula chakula kilichochafuliwa na sumu za bakteria au na vimelea maradhi. Dalili huanza kujitokeza kuanzia muda wa saa moja hadi matatu baada ya kula chakula kisichofaa. Pia wakati mwingine mtu huwa hahisi kuwa mgonjwa, hadi kupita siku kadhaa baadaye na iwapo mtu atakuwa amekula chakula kilicho na kiasi kidogo cha sumu muda wake wa kuuugua utakuwa mfupi na mara moja ataanza kujisikia vizuri. Katika hali kama hiyo mtu anapoona ana dalili hizo tulizozitaja, ni vyema amuone daktari mapema kwa ajili ya matibabu. Iwapo utakwenda kwa daktari atakuuliza maswali mengi kama vile unajisikiaje, umeanza kuumwa lini, ulikula nini hapo kabla na kama kuna mtu yoyote wa karibu yako aliye na dalili kama zako. Aidha daktari anaweza kukuandikia vipimo vya haja kubwa na ndogo ili kuona kama vijidudu maradhi hivyo ndivyo vimesababisha hali hiyo iliyokusibu au la. Pia iwapo utaona damu ndani ya kinyesi, unashauriwa kumuona daktari mara moja pasina kuchelewa.
&&&&&&&&&

Mambo mengi yanaweza kufanywa ili kuzuia vijidudu maradhi na sumu kuchafua chakula chetu. Mosi ni kusafisha vyema mikono kabla na kila mara unapotayarisha chakula na kabla ya kula, na kusafisha sehemu zote zinazotumiwa wakati wa maandalizi ya chakula. Pia madodoki na sponji za kuoshea vyombo kwa kiasi kikubwa huwa na uwezekano wa kubeba bakteria hivyo ni lazima vifaa hivyo vioshwe mara kwa mara baada ya kutumika. Vilevile tunapaswa kufunika kwa sashi au bandage sehemu yoyote yenye mchubuko au uliojikata katika mkono kabla ya kuanza kuandaa chakula. Vyakula aina ya nyama na mayai vinapaswa kupikwa vyema na kupashwa moto vizuri kabla ya kuliwa. Pia tuhakikishe kwamba majokofu au mafriji yanakuwa katika nyuzi joto 40 na freeza katika nyuzi 0 au chini ya hapo ili kuhakikisha kwamba vyakula vinahifadhiwa vyema na kuepusha muozo. Kiporo cha chakula kisikae ndani ya jokofu kwa zaidi ya siku nne, nyama haipaswi kuachwa ovyo bila ya kuhifadhiwa, na ni vyema ichemshwe kwa zaidi ya nyuzi joto 140. Pia tunapaswa kuwa waangalifu wakati wa kuhifadhi vyakula kama vile samaki na nyama mbichi kwani vinaweza kuchafuliwa kirahisi na bakteria au vimelea wa maradhi. Ni bora samaki wasivuliwe kutoka kwenye maji yaliyochafuka, na tunashauriwa kusafisha mboga mbichi na matunda kabla ya kula au kupika, na pale tunaponunua vyakula vinavyohifadhiwa ndani ya makopo, mikebe na kadhalika tunapaswa kwanza kuangalia muda wa matumizi yake unakwisha lini. Pia vyakula ambavyo vinahifadhiwa katika makopo kama vile samaki, nyama na vinginevyo tunashauriwa kuvichemsha kabla ya kuliwa na pale tunapoona kuwa makopo hayo yamefura kuliko kawaida, hiyo ni dalili kuwa vyakula hivyo vimeharibika. Hii ni kwa sababu bakteria aina ya Clostridium Botulinum anayepatikana katika vyakula vinavyosindikwa katika makopo huweza kusababisha aina ya food poisoning inayotokana na sumu ya botulism ambayo ni hatari na huua. Pia maziwa ya ng'ombe ambayo hayajapitia katika njia ya kuondolewa vijidudu inayojulikana kama pasteurization, yanapaswa kuchemshwa vizuri kabla ya kutumiwa. Itakumbukwa kuwa watoto, wazee na wale wote wenye magonjwa ya muda mrefu au wenye kinga dhaifu ya mwili huwa na hali mbaya wanapokula chakula kilichoharibika au kuchafuliwa na vimelea vya maradhi. Kwa hiyo ili kukabiliana na tatizo hili, tunapaswa kuwa makini sana kuhusiana na suala hili.

Wednesday, March 16, 2016

FAIDA ZA PAPAI

FAIDA NYINGI ZA PAPAI.

Mpapai ambao kitaalam hujulikana kama Carica papaya, ni mti wenye tunda lenye virutubisho vingi ambao una asili na hulimwa na kustawi katika nchi za kitropiki. Mpapai  hukua hadi kufikia kimo cha mita 10. Mti huu huwa na makovu ambayo hutokana na majani ya mpapai yaliyoanguka unapokua.

Mpapai ni wenye asili ya bara la Amerika ya kati na kusini lakini badae mmea wa tunda hili ulisambaa katika visiwa vya Caribbean, Florida na Baadhi ya nchi za Afrika. Leo hii papai hulimwa katika nchi za India, Australia, Indonesia, Philippines, Malaysia, U.S na Hawaii.

 Mmea huu wenye jinsia tatu: jike, dume na jikedume(hermaphrodite). Mpapai dume huzalisha poleni (mbegu dume) lakini hauzai matunda. Mpapai jike hauwezi kuzaa matunda bila kurutubishwa na poleni kutoka mpapai dume. Mpapai dumejike hujitegemea na waweza kuzaa matunda wenyewe. Na mipapai yote inayolimwa kibiashara huwa ni dumejike. Tunda la papai lina kirutubisho cha beta carotene ambacho hulipa papai rangi nzuri ya chungwa ya kung'aa.

Virutubisho katika papai
Jedwali likionyesha kiasi cha virutubisho katika gramu 100 za papai.
Aina ya kirutubisho
Kirutubisho
Kiwango kilichopo
Vitamini
Vitamini A
135ug

Vitamini E
1   ug

Vitamini C
62 mg

Thiamine
0.0mg

Niacini
0.3mg

Vitamini B 6
0.0mg

Folate
38 ug
Madini
Kalshamu
24mg

Phosphorasi
5 mg

Magnesiamu
10mg

Potasiamu
257mg

Munyu (Sodium)
3mg

Chuma
0.1mg

Zinki
0.1mg

Shaba
0.0mg

Manganizi
0.0mg
Protini muhimu
TRP(Tryptophan)
8mg

THR(Threonine)
11mg

ILE(Isoleucine)
8 mg

LEU(Leucine)
16mg

LYS(Lysine)
25mg

MET(Methionine)
2 mg

CYS(Cysteine)
5 mg

PHE(Phenylalanine)
9 mg

TYR(Tyrosine)
5mg

VAL(Valine)
10 mg

 Matumizi ya matunda na mboga za majani yamekuwa yakihusishwa na kupungua kwa athari za kiafya zisababishwazo na mfumo mpya wa maisha. Tafiti nyingi zimeonyesha kuwa kuongezeka kwa matumizi ya vyakula vitokanavyo na mimea kama papai hupunguza athari kama kuwa na uzito mkubwa, kisukari, magonjwa ya moyo na huboresha afya na kuongeza nishati mwilini. Zifuatazo ni baadhi ya faida zitokanazo na ulaji wa papai:

Tunda la papai lililowiva lina kiwango kikubwa cha Vitamini C (62mg) ukilinganisha na chungwa lenye kiwango cha 53mg katika gramu 100 za tunda. Tafiti zimeonyesha faida nyingi za vitamini C kama kuondoa sumu mwilini(sumu hizi hujulikana kama free radicals), kuimarisha kinga ya mwili na kujikinga na visababishi vya maumivu na uvimbe.

Papai hupunguza kiwango cha lehemu kwa kuwa lina Vitamini C na virutubisho vingine ambavyo huzuia kujijenga kwa lehemu katika mishipa ya damu ya ateri. Lehemu inapojikusanya kwa wingi katika ateri, mishipa hii ya damu huwa na njia nyembamba au kuziba na kusababisha kuongezeka shinikizo la damu na hata shambulizi la moyo.

Tunda hili husaidia kupunguza uzito wa mwili, papai lina fiba (nyuzi lishe) ambazo husaidia kupunguza uzito, unapokula tunda hili, fiba husababisha kujisikia umeshiba kwa hiyo mtu hupunguza kiasi cha chakula chenye nishati nyingi ambapo hupelekea kupunguza uzito wa mwili.

Afya njema ya macho hupatikana kwa kula tunda hili. Papai lina kiwango kikubwa cha Vitamini A na vitutubisho vingine kama Beta carotene ambavyo husaidia kuiweka katika hali ya afya njema ya ngozi utando ya macho, na kuzuia kudhurika kwa macho. Pia vitamini A huzuia kuharibika sehemu ya macho inayohusika na kuona kutokana na umri mkubwa na kutuepusha matatizo ya kuona.

Katika utafiti mmoja uliochapishwa katika jarida la magonjwa ya viungo(arthritis) ulionyesha kuwa, watu wanaokula vyakula vyenye kiwango kidogo cha vitamini C walikuwa katika hatari mara tatu zaidi ya kupata magonjwa ya viungo. Kula papai ni muhimu kwa afya ya mifupa yako kwa kuwa husaidia kuondoa visababishi vya uvimbe na maumivu pia lina vitamini C kwa wingi ambayo hutukinga na aina nyingi za magonjwa ya viungo.https://www.blogger.com/blogger.g?blogID=4190877296945965391#editor/target=post;postID=8284290276971163185

Tuesday, March 15, 2016

MAGONJWA YA NGOZI


Mapunye na athari kwa ngozi yako

Ni matumaini yangu kuwa hamjambo wapenzi wasomaji wa blog yetu ya watoto karibuni katika makala nyengine ya Ijue Afya Yako. Katika kuhitimisha kujadili maradhi ya ngozi leo tunaangalia maradhi ya fangasi ya mapunye yanayoshambulia kichwa ambayo kitaalamu huitwa Tinea capitis.



Aina hii ya maradhi ya fangasi hushambulia eneo la kichwa pekee ukiacha eneo la uso. Kwa maneno mengine, aina hii ya fangasi haishambulii uso bali eneo lililobaki la kichwa. Lakini je, mapunje huwashambulia kina nani zaidi? Ugonjwa huu hushambulia watu wote wa jinsia na umri wote, ingawa huonekana zaidi kwa watoto wadogo. Fangasi hawa hushambulia watoto wadogo ambao hawajafikia umri wa balehe na mara nyingi huacha kushambulia pale mtoto anapofikia umri huo wa balehe. Iwapo unataka kujua muonekano wa maradhi haya, unapaswa kujua kuwa, mapunye huweza kushambulia eneo zima la kichwa au sehemu tu ya kichwa. Eneo la ngozi ambalo lina mashambulizi ya mapunye huwa na umbo linalofanana na sarafu. Eneo hili la ngozi lililoathirika kama lina nywele, hunyonyoka na hivyo mwonekano wa mfano wa sarafu huonekana wazi hata bila kutumia jicho la kitaalamu.

Dalili zake
Ukiachilia mbali mwonekano wa mapunye kama tulivyoeleza kuna dalili nyingine za maradhi haya ambazo ni: Eneo la ngozi lililoshambuliwa kuwasha, ingawa si mara zote na kubadilika kwa rangi ya ngozi ya eneo lenye maambukizi. Ukitazama kwa makini eneo ambalo lina mashambulizi ya maradhi haya utagundua kuna vidoti vyeusi ambavyo vinaonyesha eneo ambalo nywele imeng'oka kutokana na maradhi. Dalili nyingine ya mapunye ni ngozi kubanduka kwenye eneo lenye maambukizi na pia ngozi kukauka kwenye eneo hilo. Mara nyingine usaha pia huweza kuonekana kwenye eneo la ngozi lililoshambuliwa na fangasi hawa na hali hiyo kitaalamu huitwa kerions. Kama maradhi haya yakikaa bila kutibiwa kwa muda mrefu husababisha dalili nyingine ambayo ni kuonekana kama kutoka majimaji kwenye eneo la ngozi lililoathirika pamoja na kutoka harufu mbaya kwenye eneo hilo lililoathiriwa na vimelea hivi vya fangasi. Kuna njia nyingi zinazoweza kusababisha uambukizi wa mapunye lakini ili uambukizaji huu uwezekane lazima kuwe na mazingira yanayofaa ya kuwezesha fangasi kuishi na kuhama kwa urahisi. Mazingira haya yanayofaa kuruhusu fangasi hawa kuweza kutoka kwenye kichwa cha mtu mmoja kwenda kwa mwingine huhitaji uwepo wa hali ya joto pamoja na majimaji au unyevunyevu. Watu ambao wako katika hatari ya kupata maambukizi ya mapunyeni ni wale wanaoshirikiana na wenzao vifaa vya kunyolea bila kuvisafisha vizuri na pia wanaoshirikiana vifaa vya kufanya usafi wa mwili zikiwamo taulo. Vilevile wanaotoka jasho sana hasa kichwani kwani huweza kuweka mazingira mazuri zaidi ya kuruhusu maambukizi ya ugonjwa huo yatokee kirahisi. Wale wanaofanya kazi zinazohusisha uwekaji vichwa kwenye maji yaliyotuama kwa muda mrefu na wale ambao tayari wana fangasi za kichwani kwani ni rahisi kwa fangasi hao kujirudia. Kundi jingine lililo katika hatari ya kupata ugonjwa wa Tinea capitis ni na wale watu wanaofanya usafi wa mwili kwa kutumia maji yaliyobeba vimelea vya fangasi wa mapunye, wasiojikausha vichwa baada ya kuoga au kutofanya usafi wa kichwa kwa ujumla na watu wenye maradhi yanayosababisha kushuka kwa kinga ya mwili kikiwemo kisukari. Hali kadhalika wale wanaokunywa kwa muda mrefu dawa za kuua vimelea yaani antibiotiki na pia watoto wadogo ambao hawajafikia umri wa balehe.
&&&&&&&&&&&&&&&&&&
Huwa ni rahisi sana kwa mapunye kuambukizwa kutoka kwenye kichwa cha mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia zifuatazo. Moja ni kutumia vifaa vya kunyolea kwa zaidi ya mtu mmoja bila kuvifanyia usafi wa kuua vimelea kama fangasi wa aina hii. Pili kutumia taulo au nguo ya kujikaushia kwa mtu zaidi ya mmoja hasa pale ambapo mmoja wa watumiaji hao ana maambukizi haya ya fangasi. Kutumia vifaa vya nywele kama chanuo la kuchania nywele kwa zaidi ya mtu mmoja hususan pale ambapo mmoja wa watumiaji hao ana maambukizi ya vimelea vya fangasi hawa, kugusana na mtu aliye na maambukizi tayari na pia kushirikiana mavazi aina ya kofia na mtu aliyekwisha pata maambukizi hayo.
Kuhusiana na kuutambua ugonjwa huo mara nyingi aina hii ya fangasi hugundulika kwa macho hasa kwenye maeneo ambayo fangasi hao wapo kwa wingi. Kwa kutazama ngozi ya sehemu ya kichwa iliyoathirika na maambukizi ya fangasi hao, utaweza kuona madhara yanayokukabili. Iwapo vipimo vitahitajika basi sehemu ya ngozi iliyoathirika huchukuliwa kwa ajili ya kufanya vipimo vya maabara na kuangalia aina sahihi ya fangasi na pale inapothibitika matibabu huanza.
Mara nyingi mapunye hutibika kwa dawa za kutibu fangasi za kupaka ambazo hutibu mapunye na kuyaponyesha kabisa bila kuhitaji kutumia dawa za kumeza. Hii ni kwa kuwa ni rahisi kwa dawa ya kupaka kupenya kwenye ngozi na kusababisha matokeo yanayohitajika. Matibabu ya mapunye huchukua muda mfupi lakini huonyesha matokeo mazuri na kwa bahati matibabu ya fangasi huleta matokeo chanya mara zote. Lakini huwa ni rahisi kwa maradhi hayo kurudi baada ya kumaliza matibabu kama hatua madhubuti za kujikinga na maradhi haya hazitochukuliwa. Kwa sababu hiyo, ni vizuri kwa mgonjwa wa fangasi kutumia dawa mpaka wiki mbili baada ya dalili za maradhi kutoweka. Lakini je ni vipi tunaweza kujikinga tusipatwe na ugonjwa wa mapunje?
Wapenzi wasikilizaji kama tulivyosema magonjwa mengi ya fangasi hujirudia kwa waathirika hata baada ya matibabu iwapo hawatozingatia njia sahihi za kujikinga na maradhi hayo. Kuna mbinu mbalimbali za kujilinda usipatwe na mapunye na fangasi kwa ujumla. Kwanza kabisa ni kuhakikisha kwamba mwili wako hasa kichwani muda wote ni mkavu. Hii ni kwa sababu kama tulivyosema faghasi hupenda kumea katika sehemu nyevunyevu. Pia hakikisha kwamba unaosha nguo, taulo na mashuka mara kwa mara ili kuhakikisha kwamba fangasi wanaondolewa na pia epuka kushirikiana vifaa vya kunyolea nywele hasa kama hakuna namna ya kuvisafisha na dawa maalumu ya kuua vimelea kabla hujatumia kifaa hicho. Njia nyingine ya kujikinga na maambukizi ya fangazi ni kuepuka kushirikiana katika utumiaji wa vifaa vya kufanya usafi wa mwili kama mataulo. Pia kama kazi yako inahusisha ukaaji wa muda mrefu kwenye maji basi hakikisha kwamba unakausha mwili hasa sehemu za kichwa au unaweka dawa ya kuzuia fangasi kwenye maji hayo unayotumia.
&&&&&&&&&&&&&&
Na tunahitimisha kipindi chetu cha leo kwa kuelezea faida za papai. Tunda hili lenye ladha nzuri kama sukari, siyo tu ni tamu kulila, bali pia ni chanzo kikuu cha virutubisho muhimu vinavyotoa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali, na kuukinga na maradhi tofauti. Inaelezwa kuwa papai ni kinga ya ugonjwa wa moyo unaotokana na kuziba kwa mishipa ya damu na ule unaotokana na kupatwa na kisukari. Tunaelezwa kuwa kwa kula papai mara kwa mara tunaweza kuepusha magonjwa hayo yanayosababisha kifo haraka. Pia papai limeonesha kuwa na uwezo mkubwa sana wa kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa saratani ya utumbo ambayo hutokana na mtu kuwa na matatizo katika mfumo wake wa usagaji chakula. Kwani tunda hilo huboresha mfumo mzima wa usagaji chakula na kumfanya mtu kupata choo laini na hivyo kujiepusha na madhara ya kukosa choo kwa muda mrefu ambayo humuweka katika hatari ya kupatwa na kansa ya tumbo. Watu wanaosumbuliwa na majipu au kutokwa na vimbe za ajabu ajabu pamoja na vidonda mara kwa mara, sababu kuu mara nyingi huwa ukosefu wa virutubisho muhimu vinavyopatikana kwenye tunda hili. Imegundulika kuwa, watu wenye matatizo hayo wanapotumia papai au virutubisho vyake, hupata nafuu haraka na kupona matatizo hayo. Vitamin C na Vitamin A ambayo inapatikana mwilini kutokana na kirutubisho aina ya beta-carotene kilichomo kwenye papai, ni muhimu sana kwa ajili ya kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa yanayojirudia mara kwa mara kama vile mafua, maambukizi ya sikio, kikohozi na kadhalika. Pia papai huongeza nuru ya macho kama zinavyoaminika karoti katika suala hilo. Wataalamu wa lishe wanasema kuwa, watu wanaotumia tunda hili hujipa kinga madhubuti ya macho na pia kudhibiti kasi ya kuzeeka ambayo hutokana na kuongezeka umri.
Vilevile kama wewe ni mvutaji sigara au mtu ambaye katika mazingira yako unayoishi unakumbana na moshi wa sigara, basi utumiaji wa vyakula vyenye kiwango kikubwa cha vitamin A kama papai, hukuepusha kupatwa na madhara yanayotokana na moshi wa sigara. Ulaji wa papai pia huepusha hatari ya kupatwa na ugonjwa wa saratani ya kibofu cha mkojo. Suala hilo limeeelezwa katika utafiti wa hivi karibuni uliochapishwa na Asia Pacific Journal of Clinical Nutrition. Kwa ajili hiyo wapenzi wasikilizwaji tujitahidi kula tunda la papai ili kupata faida hizi na nyinginezo, na kujiepusha na magonjwa hatari yanayosumbua watu kila siku.

games

NJIA ZA KUMWANDAA MTOTO KUWA NA UPEO MKUBWA(AKILI)

Watoto ni wepesi kushika vitu na ni waelewe sana ,wanakuwa kulingana na malezi wanayopewa na wazazi. Wazazi wengi wanaamini mtoto huanza kufunzwa akiwa miaka 3-4 hapana tunakosea sana wenzetu nchi zilizo endelea wanaanza funza watoto wakiwa na miezi 6 hufunzwa kila vitu kulingana na umri mfano kusomewa vitabu mzazi unaweza ukaona haelewi hapana kichwa kinazoea kile anachofunzwa mara kwa mara  .


Ukimwandalia mtoto msingi mzuri  tangu udogoni basi ana nafasi nzuri ya kuwa na upeo(akili) na  uwelewa mkubwa.Wazazi wengi wanaachia watoto wakiamini kila kitu watafunzwa shule ,hapana ni makosa mzazi inakubidi uchukue nafasi yako  pia  kuhakikisha unampa mwongozo bora mtoto .
Watoto wengine ni wazito kuelewa ️au kushika vitu kwa haraka hivyo vizuri akanza kufunzwa mapema.Maandalizi mazuri kwa mtoto yatamjenga kiakili na kumfanya kuwa bright. Hakuna mtoto mjinga duniani ni wazazi tu kukosea kuto kuwapa misingi bora watoto tangu wakiwa na umri mdogo.


ujue ratiba yake akitoka shule anatakiwa kufanya nini,atacheza na wenzake kupumzisha kichwa kumbuka michezo ni muhimu kiafya,baada ya michezo afanye kazi za shule kwa kumsaidia,muulize leo shule wamefanya nini ?kipi kilimfurahisha? nini kilimkasirisha? ,masomo yalikuwaje itakusaidia kujua maendeleo yake ya shule na mahusiano yake na walimu na wanafunzi wenzake ,na unaweza mwelekeza homework yake

Wale wadogo wasio enda shule miezi 9-mpaka miaka 3 nao vile vile anatakiwa tengewa mda Wake ,anavyozidi kukua anazoea ile ratiba na kukaa kichwani kwamba nitacheza ila kunamda nitakaa kusoma hata kama dakika 10-20

TUPANDE MITI YA MATUNDA

TUPANDE MITI YA MATUNDA KUKIDHI KIWANGO KINACHOHITAJIKA KWA SIKU.

Kila hatua utakayochukua ya kula zaidi matunda na mboga mboga, itakusaidia wewe na familia yako kuwa na afya njema. Hii ni kwa sababu matunda na mboga za majani yana viini lishe muhimu ambavyo husaidia ufanyaji kazi wa mifumo ya miili yetu na kutukinga na aina mbali mbali za magonjwa.

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO, ni kuwa ulaji wa angalau gramu 400(pungufu kidogo ya nusu kilo) za matunda na mboga kwa siku zinatuepusha na hatari ya kupata magonjwa yanayosumbua jamii nyingi duniani hivi leo. Magonjwa haya zaidi ni yale yasiyo ya
uambukizi kama kisukari, shinikizo la damu, kiharusi na mengine mengi. Pia ulaji wa matunda na mboga mboga utatusaidia kupata  viini lishe kama fiba, vitamini, madini katika viwango sahihi vinavyohitajika kwa siku.

Katika nchi zinazoendelea ambapo walio wengi wanaishi chini ya dola moja kwa siku, ni vigumu kuweza kumudu kufikia kiwango kilichopendekezwa na shirika la afya duniani, lakini hii isitufanye kushindwa kumudu kiwango kilichopendekezwa. Tunaweza kujitosheleza kwa matunda na mboga za majani kwa kuotesha miti ya matunda mbali mbali majumbani mwetu, pia kuwa na bustani za mboga mboga. Hii itatusaidia kuweza kufikia kiwango kinachopendekezwa na shirika la afya WHO na kuboresha afya zetu.

Ili kuboresha kiwango kinachohitajika cha matunda na mboga mboga, basi hatuna budi kufanya

yafuatayo:-
  • Tuhakikishe kuwa nyumbani kwetu hapakosekani bustani za mboga na matunda.
  • Kila wakati hakikisha katika mlo wako haukosi mboga za majani.
  • Hakikisha haukosi matunda ya kila msimu, mfano embe, nanasi, chungwa, mastafeli, papai, fenesi,parachichi na mengineyo mengineyo mengi.
  • Kula aina tofauti za matunda na mboga za majani

ATHARI ZA SPIKA ZA MASIKIONI

SPIKA ZA MASIKIONI ZAWEZA KUSABABISHA UZIWI.

Sauti kutokana na matumizi mabaya ya spika za masikioni (earphones & headphones) zaweza kutuweka katika hatari ya kupata uziwi. Katika zama hizi za maendeleo ya digitali, kumekuwepo ongezeko la matumizi la vifaa vya kielektroniki kama rununu, runinga na kompyuta. Matumizi ya vifaa hivi huambatana na spika za mezani pamoja na spika za masikioni ili kumraisishia mtumiaji kusikiliza na kufurahia muziki. Spika za masikioni zimetengenezwa ili kumuwezesha mtumiaji kusikiliza sauti kutoka katika kifaa chake wakati wowote atakapohitaji na hata kama amezungukwa na mazingira yenye
kelele.

Usikilizaji wa sauti ya juu au sauti kubwa kwa kutumia spika za masikioni kwa muda mrefu kunaweza kupelekea kupata uziwi pia hata uziwi wa moja kwa moja. Usikilizaji huu wa sauti kubwa ni hatari zaidi kwa watoto na vijana kwa kuwa hupendelea kusikiliza muziki kwa sauti ya juu aidha nyumbani au katika vilabu vya muziki, kwenye magari na hata kwa kutumia spika za masikioni. Sauti hupimwa kwa kutumia skeli ijulikanayo kama decibel (dB).Mfano mtu anayeongea kwa sauti ya chini ni kadirio la 30 dB.

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani (WHO), kupitia takwimu zilizopatikana katika nchi zenye kipato cha kati zinaonyesha kuwa, miongoni mwa wale walio na umri kati ya miaka 13-35,karibu asilimia 50 husikiliza sauti katika kiwango kisicho salama kwa kutumia vifaa vyao binafsi vya sauti na asilimia 40 huwa katika kiwango kisicho salama cha sauti wakiwa katika kumbi za starehe. Shirika la afya (WHO) limeainisha kuwa, kukaa eneo lenye kiwango cha sauti kuanzia 85dB kwa masaa nane au 100dB kwa dakika 15 kuwa siyo salama. Inakadiriwa kuwa 1.1bilioni ya walio chini ya miaka ishirini(teenagers) na vijana wako katika hatari ya kupoteza usikivu kutokana na matumizi ya vifaa vya sauti zikiwemo simu za mkononi(smartphones) zinazoambatana na spika za masikioni.

Kusikiliza isivyo salama itategemea kiwango cha sauti, muda ambao utasikiliza na ni mara ngapi unasikiliza.

Inashauriwa kuwa kiwango cha juu cha sauti katika maeneo ya kazi ni 85dB na isizidi masaa nane kwa siku. Wafanyakazi wa vilabu vya usiku na baa mara nyingi huwa katika kiwango cha juu cha sauti na wanashauriwa kupunguza masaa ya kazi. Kwa mfano katika klabu za usiku, huwa na kiwango cha 100dB kwa hiyo itakuwa salama kwa masikio yetu endapo tutakaa katika kumbi hizo kwa dakika 15 tu.

Walio chini ya umri wa miaka ishirini na vijana waweza kujilinda kwa kuweka tuni za chini katika vifaa vyao vya sauti au kuvaa vifaa vya kuzuia sauti wawapo maeneo yenye sauti kubwa ili kuepuka kupata uziwi. Pia waweza kupunguza muda watakaokaa katika eneo lenye sauti kubwa au kuepuka matumizi ya mara kwa mara au siku chache za kutumia vifaa vya sauti kama spika za masikioni

Sunday, March 13, 2016

FAIDA ZA MATIKITI MAJI

FAIDA ZA TIKITI MAJI.

Tikiti maji ni tunda ambalo kisayansi hujulikana kama Citrullus lanatus katika familia yaCucurbitaceae, ambalo mmea wake hutoa maua na humea kwa kutambaa. Mmea huu ambao hutoa matunda makubwa yaliyo na umbo la tufe au yai, asili yake ni huko kusini mwa Afrika.

Ushahidi wa kihistoria ulionyesha kuwa mmea huu ulilimwa huko Misri tangu milenia ya pili BC, na katika karne ya kumi AD mmea wa tikiti maji ulikuwa umesambaa huko bara Hindi hata Mashariki ya mbali.Lakini hapo badae ulimaji
wake ulifika huko Ulaya ya kusini na kusambaa duniani kote.Tafiti nyingi zimekuwa zikifanyika kujaribu kuzalisha mbegu za tikiki zenye kukabiliana na magonjwa yashambuliayo mmea huu.

Ijapokuwa watu wengi huamini kuwa tikiti maji ni tunda lililo na maji na sukari peke yake, lakini ukweli ni kuwa tunda hili lina aina nyingi ya virutubisho , mfano vitamini, madini na viondoa sumu(antioxidants).

Jedwali likionyesha kiasi cha virutubisho katika gramu 100 za tikiti maji.
Aina ya kirutubisho
Kirutubisho
Kiwango kilichopo
Vitamini
Vitamini A
28µg
Vitamini E
0.0 µg
Vitamini C
8.1mg
Thiamine
0.03mg
Niacini
0.2mg
Vitamini B 6
0.045mg
Folic acid
3mg
Madini
Kalshamu
7mg
Phosphorasi
11mg
Magnesiamu
10mg
Potasiamu
112mg
Munyu (Sodium)
1mg
Chuma
0.2
Zinki
0.1mg
Shaba
0.0mg
Manganizi
0.0mg
Protini muhimu
TRP(Tryptophan)
7.0mg
THR(Threonine)
27mg
ILE(Isoleucine)
19mg
LEU(Leucine)
18mg
LYS(Lysine)
62mg
MET(Methionine)
6mg
CYS(Cysteine)
2mg
PHE(Phenylalanine)
15mg
TYR(Tyrosine)
12mg
VAL(Valine)
16mg
ARG(Arginine)
59mg
HIS(Histidine)
6mg

Mbali na virutubisho vilivyoonyeshwa katika jedwali, tunda hili la tikiti maji pia lina viondoa sumu kama flavonoids, carotenoids na triterpenoids pia kiasi kikubwa cha maji,na virutubisho hivi hulifanya tunda hili kuwa na sifa ya vyakula vyenye faida kubwa mwilini.

Tafiti nyingi zimeonyesha kuwa, kuongeza matumizi ya vyakula vitokanavyo na mimea kama tikiti maji,matunda mengine na mbogamboga hupunguza hatari ya kupata magonjwa, kuboresha maisha na kuongeza umri wa kuishi. Twaweza kuepukana na magonjwa kama uzito mkubwa(obesity),kisukari na magonjwa ya moyo. Ulaji wa vyakula hivi humfanya mtu kuwa na afya njema,ngozi yenye afya,nywele na uzito ulio wa wastani.

Tunda hili lenye lycopene ambayo ni kiondoa sumu(antioxidant) na ambayo hulipa tunda hili rangi ya kupendeza iliyo nyekundu au pink, pia hupatikana katika nyanya na matunda mengine yaliyo na rangi nyekundu.

Tafiti za awali zimeonyesha kuwa watu walao matunda kama tikiti na mengineyo yenyelycopene kwa wingi waweza kuwa na nafasi ndogo ya kupata maradhi ya saratani hususani saratani ya tezi dume. Lakini hapajakuwepo kwa ushahidi ulio thabiti  kuonyesha uhusiano uliopo kati ya saratani ya tezi dume na utumiaji wa matunda yenye lycopene ili kuweza kutambuliwa na mamlaka za chakula na tiba.

Katika utafiti mmoja uliochapishwa mwaka 2013 katika jarida la Kimarekani la shinikizo la damu, ulionyesha ulaji wa tikiti maji kwa watu wazima walio na uzito mkubwa uliweza kupunguza shinikizo la damu la aota (aortic BP).

L-citrulline ni aina ya protini iliyo katika tikiti maji na ambayo hubadilishwa mwilini katika figo na kuwa protini ijulikanayo kama L-arginineL-citrulline pia huongeza utengenezwaji wa nitric oxide, ambayo hufanya mishipa ya damu kutokukakamaa na kuboresha mzunguko wa damu mwilini na hii ndiyo sababu ya kupungua kwa shinikizo la damu. Tunda hili limejipatia umaarufu kwa wale walio katika ndoa,kwa kuwanitric oxide huongeza pia mzunguko wa damu katika viungo vya uzazi, kwa hiyo wale walio na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume kwa kiwango kidogo na kati, waweza kufaidika na tunda hili.

Kwa wana michezo ulaji wa tunda hili au juisi yake ni wa faida kubwa kwa kuwa husaidia kupunguza maumivu ya misuli na kuondokana na uchovu kwa haraka baada ya mazoezi au michezo ya kutumia nguvu. Watafiti wanaamini kuwa hii ni kwa sababu ya uwepo wa protini ya L-citrulline katika tikiti maji.

Tikiti maji ni tunda muhimu katika kurekebisha mmeng’enyo. Kwa kuwa  tunda hili limetengenezwa na kiasi kikubwa cha maji na fiba husaidia kuondoa matatizo ya kukosa choo (constipation) na kuboresha mmeng’enyo wa chakula tumboni. Pia kwa kuwa tunda hili lina asilimia 92 ya maji na madini, huwa ni chaguo zuri kwa wagonjwa wenye upungufu wa maji mwilini.

Hatari ya kupata ugonjwa wa pumu ni mdogo kwa wale wanaokula aina fulani ya virutubisho. Katika moja ya virutubisho hivi ni vitamini C ambayo hupatikana katika aina nyingi za matunda na mbogamboga  likiwemo tikiti maji.

Tikiti maji husaidia afya ya ngozi kwa kuwa lina vitamini A na C. Vitamini A husaidia katika ukuaji wa tishu za mwili,zikiwemo ngozi na nywele. Vitamini C husaidia katika utengenezaji wa kolageni mwilini na husaidia kupona haraka kwa tishu zilizo na majeraha ikiwemo ngozi.

Tahadhari
Tikiti maji siyo lishe iliyokamilika peke yake, pia siyo tiba itakayokufanya kuacha kufuata ushauri wa daktari. Ni vema basi kuhakikisha tunakula mlo ulio kamilika ili kujenga afya bora. Tunapopata matatizo mbali mbali ya kiafya ni vizuri pia kuonana na wataalamu wa afya kwa ajili ya utafiti, ushauri na kupata tiba iliyo sahihi.

FAIDA ZA PARACHICHI

FAIDA ZA PARACHICHI


Parachichi ni tunda ambalo mti wake hujulikana kisayansi kama Persea amerikana.  Tunda hili lina aminika kuwa na asili kutoka jimbo la Puebla, bara Amerika ya kusini kunako nchi ya Mexico. Ushahidi wa kale kabisa, takribani miaka 10000 BC umeonyesha parachichi lilitumika katika jimbo la Puebla nchini Mexico. Lakini kutokana na faida nyingi kiafya zipatikanazo kwa ulaji wa tunda hili, tunda hili sasa hupatikana na kutumika kwa lishe sehemu nyingi duniani hususani barani Afrika.

Parachichi ni tunda la pekee ukilinganisha na matunda mengine, kimsingi matunda mengine huwa yana wanga(carbohydrate) kwa wingi, wakati parachichi lina aina ya mafuta ambayo yana faida kwa afya.

Jedwali likionyesha kiasi cha virutubisho katika gramu 100 za
parachichi.
Aina ya kirutubisho
Kirutubisho
Kiwango kilichopo
Vitamini
Vitamini A
7ug

Vitamini E
2.1ug

Vitamini C
10mg

Thiamine
0.1mg

Niacini
1.7mg

Vitamini B 6
0.3mg

Folic acid
81ug
Madini
Kalshamu
12mg

Phosphorasi
52mg

Magnesiamu
29mg

Potasiamu
599mg

Munyu (Sodium)
7mg

Chuma
0.6mg

Zinki
0.6mg

Shaba
0.2mg

Manganizi
0.1mg
Protini muhimu
TRP(Tryptophan)
25mg

THR(Threonine)
73mg

ILE(Isoleucine)
84mg

LEU(Leucine)
143mg

LYS(Lysine)
132mg

MET(Methionine)
30mg

CYS(Cysteine)
27mg

PHE(Phenylalanine)
232mg

TYR(Tyrosine)
49mg

VAL(Valine)
107mg

ARG(Arginine)
88mg

HIS(Histidine)
49mg

Parachichi katika tafiti nyingi limeonekana kuwa na faida katika afya ya moyo. Wagonjwa wa moyo wamekuwa katika makatazo ya kutumia aina ya mafuta ambayo yamekuwa yakichangia kuongezeka kwa lehemu katika damu(mafuta hayo kitaalam kama polysaturated fat), na kuongeza matumizi ya mafuta yasiyoongeza lehemu katika damu (monosaturated fat). Parachichi ni chanzo kizuri cha mafuta yasiyoongeza lehemu katika damu. Utafiti unaonyesha kuwa matumizi ya mafuta haya  katika parachi hupunguza lehemu iliyo hatari ( kitaalam kama, Low density lipoprotein), na huchangia katika ongezeko la lehemu isiyo hatari( High density lipoprotein).
Madini ya Potasiamu ni aina ambayo huwa watu hawapati ya kutosha kutoka katika vyakula. Parachichi lina kiwango kikubwa cha madini ya potassium kuliko ndizi. Tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa matumizi ya madini haya huambatana na kupungua kwa shinikizo la damu, shinikizo la juu la damu laweza kupelekea mtu kupata kiharusi, shambulizi la moyo hata figo kushindwa kufanya kazi.

Parachichi lina kiwango kikubwa cha fiba. Fiba ni kirutubisho kutoka katika vyakula vya jamii ya mimea, fiba huwa hazimeng’enywi tumboni lakini huwa zina umuhimu mkubwa sana, kama kusaidia kupunguza uzito wa mwili, kusaidia urekebishaji wa kiwango cha sukari mwilini na kupunguza hatari ya kupata magonjwa mengi mwilini. Kuna aina fulani ya fiba ambazo huwa ni virutubisho kwa ajili ya bakteria wenye faida tumboni, hii huimarisha kinga ya mwili na kusaidia mwili kufanya kazi katika kiwango kinachotakiwa. Kwa kuwa parachichi lina kiwango kikubwa cha fiba, husaidia kuboresha mmeng’enyona kupata choo katika hali ya kawaida.

Aina ya mafuta na virutubisho tulivyoviona awali katika parachichi vinasaidia afya ya ngozi yako. Husaidia ngozi yako kutokuwa kavu na kuwa na unyevu unaotakiwa na kuifanya ngozi kuwa laini na yenye afya. Vitamini C husaidia katika kusaidia uponaji haraka wa ngozi na kujijenga upya kwa seli za ngozi zilizoharibika,husaidia kujengaelastini na collageni ambazo ni muhimu katika ngozi. Uwepo wa virutubisho viondoavyo sumu(antioxidants) katika parachichi kama carotenoidi na vitamini E, hutusaidia kutukinga na mionzi mikali ya jua, kwa hiyo huzuia makunyanzi katika ngozi na kuifanya ngozi yako kuwa na mwonekano mzuri wakati wote.

Tunda hili ni lishe bora kwa wale wenye kisukari. Parachichi lina kiwango kidogo cha sukari ukilinganisha na matunda mengine. Pia uwepo wa mafuta aina ya ‘monosaturated’ husaidia kuboresha ufanyaji kazi wa homoni ya insulini, katika urekebishaji wa kiwango cha sukari mwilini. Faida nyingine ni kuwa Vitamini C  katika parachichi husaidia kuimarisha mishipa ya damu na kuboresha kinga ya mwili ambayo ni faida kubwa kwa wagonjwa wenye kisukari.

Faida katika afya ya uzazi ni dhahiri. Parachichi lina Vitamini E ambayo ni “antioxidant”  Potasiamu, Vitamini B6,Vitamini C ambazo hutusaidia kutukinga na magonjwa ya moyo hata yale ya kisukari. Chochote kile kinachosaidia afya ya moyo pia husaidia afya ya uzazi. Wanaume wenye magonjwa ya moyo na kisukari huwa tatizo kubwa la upungufu wa nguvu za kiume.

Parachichi pia limeonekana kuwa na faida nyingi katika kuboresha afya ya macho, viungo vya mwili na nyinginezo nyingi. Katika utafiti mmoja uko Marekani, ulionyesha kuwa watu walao parachichi walionekana kuwa na afya bora ukilinganisha na wale wasiokula parachichi. Waliokula parachichi hawakupatwa  na matatizo ya mmeng’enyo ukilinganisha na wale wasiokula. Matatizo ya mmeng’enyo huchangia watu kupatwa na magonjwa ya moyo na kisukari.